Social Icons

Alhamisi, 26 Septemba 2013

Maoni juu ya Wachagga

Ingawa wanaume wa kichagga hupendelea kufanya kazi mbali na kwao, wake zao hukaa nyumbani (Moshi) na hufuga ngombe na kazi za shambani. ila kwa sasa kutokana na ugonjwa wa ukimwi tabia hii imepungua miongon mwao. Wanawake wa kichagga (hasa kutoka Rombo) hujulikana kama wafanyakazi hodari. Huchangia sana katika mapato ya nyumbani na chakula. Ingawa kipato cha wachaga ni kikubwa kulinganisha na cha makabila mengine, takwimu zinaonyesha watoto wa mkoa wa Kilimanjaro kuwa kuongoza kwa utapiamlo. Sababu kubwa ya watoto kuwa na utapiamlo kunatokana na wazazi kujali zaidi kazi kuliko muda wa kuwahudumia watoto. Wengi wa wototo ni wale ambao wazazi wao ni watu wapombe na kipato chao kinaishia kilabuni. Utaona kwamba uchagani kuna vilabu vingi vya pombe na vinaongezeka kwa sababu imekuwa nibiashara kubwa. Karibu kila kaya kumi natano kuna kila cha pombe na kiwango cha chini kabisa cha pombe inayouzwa kwa siku katika vilabu hivyo si chini ya dede sita au lita mia moja. Pombe ni sababu moja ya watoto kuwa na utapiamlo Hii inawezekana kuwa matunda ya wazazi kutowalisha watoto wao chakula cha kutosha au chakula bora. Kuna sehemu nyingine za Uchaggani kama Old Moshi na Kibosho ambapo watoto wadogo hupewa pombe ya mbege asubuhi mchana na jioni. Sababu nyingi ni kazi; mama wa kichagga anaweza kushinda shambani kutwa na hawana desturi ya kubeba watoto mgongoni kwenda nao shambani hivyo wanakuwa nyumbani ama wenyewe au na mayaya. Mfano ulio dhahiri ni nyakati za asubuhi na mapema kwenye vyombo vya usafiri karibu robo tatu ya abiria ni wanawake wakienda katika shuguli za kibiashara na kilimo na vivyo hivyo nyakati za jioni wakirudi majumbani. Hao ni nje ya wale wanaotumia usafiri wa miguu ambao ni wengi zaidi. Pia baadhi ya wamama wa kichaga wanawajali waume zao zaidi kwani nyama nzuri ni ya baba. Kuepuka gharama baba ataandaliwa chakula kizuri tofauti na chakulawalichoandaliwa watoto japo ni chakula kilekile.pia wachaga wamekua na desturi ya kuwaenzi wazee wao walio tangulia mbele za haki kwa kuwatambikia kwa pombe na nyama za mbuzi pale tu wanapo rudi nyumbani ifikapo mwezi desemba. hili limekua ni swala la kawaida sana na halipingiki. wengi wao huwa wanarudi na magari ndio sababu utaona ya kwambwa kila ifikapo mwezi desemba kila mwaka foleni za magari zimekua zikiongezeka kutokana na wachaga kurudi nyumbani msimu wa sikukuu. wengi wao wamekua wakitoka sehemu mbalimbali za nchi na hata nje ya nchi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni