Social Icons

Ijumaa, 10 Julai 2015

Baadhi ya maneno ya kichaga

NENO NA MAANA YAKE
Shimboni Shikamoo --(Habari yako?)
Shimboni mae/mbe Shikamoo mama/baba?
Nasicha -- Nzuri
Aika --Ahsante
*mae/mbe yanaweza kuwekwa mbele ya neno lolote la salamu m.f.) "Aika mae" "Aika mbe" Aika mana -- Ahsante mtoto
Rakucha,lakucha-- Usiku mwema
Chamecha Pole na...(hasa kwa safari)
Otana -- Pole na kazi.
Okora mae -Ahsante mama kwa kunipikia chakula
(Okora mae lipo ila huwezi kusema "Okora mbe" useme tu "Aika mbe" kama baba akipika chakula labda)
Nokyelaonacho? Nukelaho u? - Unaitwa nani?(hii inategemea ni mchaga wawapi)
Ngikyelao? Njikelaho? ~~~ Naitwa ~~~
Oroka, Horoka-- Simama
Ramia, Damia-- Kaa
Tikira --Sogea Shinde! Nnde-- Twende!
Ngicho njaa mae , Njiicho Njaa mae-- Nina njaa mama
Ngacho gicho kie , njiicho njichokie -- Nimechoka
Gayuja mae, Ngaihuda mae- Nimeshiba mama
Ngicho nbeyo,njiicho mbeo-- Nina baridi
Ngicho mrike,njiicho mrike Ninasikia joto
maruwa-- maziwa
(Ruwa ina maana ya Mungu kwao katika kichaga ila hapa "maruwa" halihusiani na Ruwa)
memba--Ndizi
Maimba --mahindi
mbuya --rafiki

Alhamisi, 26 Septemba 2013

Maoni juu ya Wachagga

Ingawa wanaume wa kichagga hupendelea kufanya kazi mbali na kwao, wake zao hukaa nyumbani (Moshi) na hufuga ngombe na kazi za shambani. ila kwa sasa kutokana na ugonjwa wa ukimwi tabia hii imepungua miongon mwao. Wanawake wa kichagga (hasa kutoka Rombo) hujulikana kama wafanyakazi hodari. Huchangia sana katika mapato ya nyumbani na chakula. Ingawa kipato cha wachaga ni kikubwa kulinganisha na cha makabila mengine, takwimu zinaonyesha watoto wa mkoa wa Kilimanjaro kuwa kuongoza kwa utapiamlo. Sababu kubwa ya watoto kuwa na utapiamlo kunatokana na wazazi kujali zaidi kazi kuliko muda wa kuwahudumia watoto. Wengi wa wototo ni wale ambao wazazi wao ni watu wapombe na kipato chao kinaishia kilabuni. Utaona kwamba uchagani kuna vilabu vingi vya pombe na vinaongezeka kwa sababu imekuwa nibiashara kubwa. Karibu kila kaya kumi natano kuna kila cha pombe na kiwango cha chini kabisa cha pombe inayouzwa kwa siku katika vilabu hivyo si chini ya dede sita au lita mia moja. Pombe ni sababu moja ya watoto kuwa na utapiamlo Hii inawezekana kuwa matunda ya wazazi kutowalisha watoto wao chakula cha kutosha au chakula bora. Kuna sehemu nyingine za Uchaggani kama Old Moshi na Kibosho ambapo watoto wadogo hupewa pombe ya mbege asubuhi mchana na jioni. Sababu nyingi ni kazi; mama wa kichagga anaweza kushinda shambani kutwa na hawana desturi ya kubeba watoto mgongoni kwenda nao shambani hivyo wanakuwa nyumbani ama wenyewe au na mayaya. Mfano ulio dhahiri ni nyakati za asubuhi na mapema kwenye vyombo vya usafiri karibu robo tatu ya abiria ni wanawake wakienda katika shuguli za kibiashara na kilimo na vivyo hivyo nyakati za jioni wakirudi majumbani. Hao ni nje ya wale wanaotumia usafiri wa miguu ambao ni wengi zaidi. Pia baadhi ya wamama wa kichaga wanawajali waume zao zaidi kwani nyama nzuri ni ya baba. Kuepuka gharama baba ataandaliwa chakula kizuri tofauti na chakulawalichoandaliwa watoto japo ni chakula kilekile.pia wachaga wamekua na desturi ya kuwaenzi wazee wao walio tangulia mbele za haki kwa kuwatambikia kwa pombe na nyama za mbuzi pale tu wanapo rudi nyumbani ifikapo mwezi desemba. hili limekua ni swala la kawaida sana na halipingiki. wengi wao huwa wanarudi na magari ndio sababu utaona ya kwambwa kila ifikapo mwezi desemba kila mwaka foleni za magari zimekua zikiongezeka kutokana na wachaga kurudi nyumbani msimu wa sikukuu. wengi wao wamekua wakitoka sehemu mbalimbali za nchi na hata nje ya nchi

Ardhi

Ingawa ardhi ni msingi wa maendeleo kwa watu wote, kwa wachagga, ardhi ni mali sana kwa sababu kilimo chao ni cha mazao ya kudumu kama kahawa na ndizi hukaa shambani kwa muda wa miaka mingi. Mojawapo ya urithi wapewayo watoto ni "kihamba". Hii ni sehemu ya ardhi ambayo mtoto anategemewa atajenga na kuanzisha familia yake. Bahati mbaya watoto wa kike walikuwa hawapewi kipaumbele katika ugawanaji wa vihamba. Uhaba wa ardhi uchagani ulipelekea wachagga wengi kuhamia mikoa mingine. Hivi leo utakuta wachagga wakiishi Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya nk wakiwa wamepanda migomba yao na kuendesha biashara za maduka ya vyakula. Ukienda kwenye mikoa hii utakuta wamejenga jamii zao na vyama vyao vya kusaidiana wakati wa sherehe au matatizo. Aidha hata pombe ya mbege utaweza kuikuta katika makusanyio ya wachaga mikoani mbali mbali.

Utawala wa jadi ya Wachagga

Watawala wa kichagga waliitwa "Mangi". Hawa walihodhi mashamba, ngombe na waliheshimiwa kama viongozi wa kikabila. Walikuwa na nguvu za kisiasa na utajiri. Baadhi ya ma-mangi mashuhuri katika historia ni kama Mangi Rindi aliyeingia mikataba na wakoloni (wajerumani), Mangi Sina wa kibosho - anajulikana kwa uhodari wake wa vita katika kupigana na wamachame na kupora ngombe na mazao yao na Mangi Marealle wa Marangu na Vunjo. Wakoloni walipokuja Kilimanjaro waliingia mikataba na viongozi hawa wa kikabila ili kuweza kuweka misingi yao ya kikoloni. Pia ndugu na watoto wa ma-Mangi walikuwa wa kwanza kupata elimu ya kikoloni, kwa hiyo waliweza kushirikishwa katika serikali za kwanza. Hawa pia wanaaminika walikuwa ni kama mabepari wa kwanza wa ki-jadi, maana walifanyiwa kazi na watu wengine wakati wao ma-mangi wamekaa kuhesabu mali zao. Usemi maarufu wa "u-Mangi-meza" inawezekana kuwa umetokana na watawala hawa wa kichagga.

Wachagga na muhogo

Inasemekana kuwa "mchagga halisi, hali muhogo - akila muhogo atakufa". Usemi huu umetokana na historia ya mababu kuwa wachagga waliopanda mihogo Kilimanjaro enzi za kale walikufa baada ya kuila. Historia hiyo yaweza kuwa ya ukweli kwa sababu aina nyingi za mihogo zinajenga sumu ya sianidi ndani yao; watu waliozoea kutumia mihogo huwa na njia za kuondoa sumu kwa kwa kuiloweka mihogo katika maji kwa muda. Lakini kama Wachagga wale wa zamani hasa wa Machame walifanya jaribio bila kujua mbinu ya kuondoa sumu ajali iliweza kutokea. Cha kushangaza ni kwamba huko huko Kilimanjaro, majirani na watani wa wachagga yaani Wapare walikuwa wameshazoea mihogo na ilikuja kuwa moja ya chakula chao kikuu.

Majina ya Kichagga

Majina ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu gani ya Uchaga, japo si lazima kuwa hivyo: mfano familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama Kimaro, Swai, Massawe, Mushi, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi, Meena hutoka Machame. Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kileo, Kimambo, Tesha wanatoka Old Moshi na Vunjo. Kavishe,Mariki, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Massawe, Lyaruu, Makyao, Mowo, Lamtey, Tairo, Mramba, Kauki wanatoka Rombo. Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa, Mtui, Moshi, Meela, Minja, Njau wanatoka Marangu Kilema na old Moshi. Rite, Makule, Minja, Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo, Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo, Towo, Mkony, Temba na kadhalika hutoka Kibosho.
Wachagga wengi hupenda kurudi nyumbani kipindi cha Krismasi, ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu. Ingawa wengi hudhani kwamba Wachagga wameathiriwa sana na dini ya Ukristo kwa kuwa wengi wao ni Wakristo na hiki huwa ni kipindi cha likizo kwao, inaaminika pia kuwa kurudi kwao Uchagani wakati wa Krismasi ni pamoja na kutembelea ndugu zao na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka baada ya kazi nyingi za kutafuta pesa kwa mwaka mzima.

Ulaji kiti-moto

Pamoja na kilimo cha mazao, wachagga hupendelea sana kufuga nguruwe. Tabia ya kula nyama ya nguruwe ijulikanayo leo kwa jina la "kiti moto" ni moja ya mambo yaliyoenezwa na wachagga. Ulaji wa "kiti moto" haukupendeza baadhi ya wenyeji wa Pwani kama Dar es Salaam ambapo wachagga walihamia, kwani wakaaji wengi wa Pwani ni Waislamu kwa hiyo nguruwe kwao ni haramu. Wakazi wa Dar es Salaam watokao makabila mengine na wasiyo waisalmu kwao kula nguruwe ilikuwa "ruksa".